Skip to main content

UNMIL yasaidia shughuli za uokozi wa waliozama na meli nchini Liberia

UNMIL yasaidia shughuli za uokozi wa waliozama na meli nchini Liberia

Kikozi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Liberia kinasaidia katika juhudi za uokozi nchini Liberia baada ya meli kuzama.

Kikosi hicho UNMIL kimejiunga na juhudi za uokozi katika pwani ya magharibi mwa Afrika baada ya meli iliyokuwa na abiria kuzama kuhu baadhi ya watu wakiarifiwa kutojulikana waliko. UNMIL imetuma helkopta mbili leo asubuhi ili kusaidia katika kuwasaka manusura baada ya ujumbe kutoka eneo la Hevea karibu na bandari ya Liberia eneo linalopakana na Ivory Coast.

Kwa mujibu wa duru za nchi hiyo watu 11 hawajulikani waliko na wengine 16 wameokolewa. Meli hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka mji mkuu wa Liberia Monrovia kuelekea Harper.