Skip to main content

Mwanamuziki maarufu Anne Lennox ameteuliwa kuwa balozi mwema wa UNAIDS

Mwanamuziki maarufu Anne Lennox ameteuliwa kuwa balozi mwema wa UNAIDS

Mwimbaji mashuhuri, mtunzi na mtetezi wa haki za wanawake kutoka Scotland Annie Lenoz ameteuliwa kuwa balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS.

Bi Lennox amesema dhulma kwa mamilioni ya wanawake ni mambo wanayokabiliana nayo kila siku na ni jambo ambalo halikubaliki.Na kama tunatarajia kumaliza mzunguko wa dhiki zilinazosababishwa na ukimwi kwa binadamu basi ni lazima tushughulikie haki za watoto na wanawake na kubadili hali ya kuwafanya wao kuwa raia wa daraja la pili.

Awali Bi Lennox alishiriki pamoja na UNAIDS katika utekelezaji wa mpango wa miaka mitano wenye lengo la kuleta usawa na kukabiliana na ukiukaji wa haki za binadamu.