Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa upinzani waonywa dhidi ya ghasia zozote zitakazotokea nchini Burundi

Viongozi wa upinzani waonywa dhidi ya ghasia zozote zitakazotokea nchini Burundi

Serikali ya Burundi kupitia mawaziri wa ulinzi na usalama wa raia wametoa onyo kali kwa muungano wa vyama vya upinzani nchini humo.

Upinzani huo ni muungano wa vyama 13 vilivyopinga matokeo ya uchaguzi wa madiwani uliofanyika 24 mwezi uliopita. Serikali imesema vikosi vya usalama havitofumbia macho yeyote anayekusudia kuzusha ghasia na kuvuruga usalama.

Jana wagombea watano wa Urais walijitoa kwenye kinyang'anyoro wakidai uchaguzi umeghubikwa na wizi wa kura. Wiki jana wagombea hao walitaka tume ya uchaguzi ivunjwe. Charles Petrie ni mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi je UM unafanya nini kuhusu hali hiyo?

(SAUTI YA  PETRIE BURUNDI)