Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa UM yuko ziarani nchini Uganda

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa UM yuko ziarani nchini Uganda

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amewasili nchini Uganda hii leo na atakuwepo hadi Jumamosi Juni tano wiki hii.

Akiwa nchini humo Bi Pillay atakuwa na mazungumzo na maafisa mbalimbali wa serikali, jumuiya za kijamii na wdau wengine kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Uganda likiwemo la matatizo ynayolikabili jimbo la Karamoja kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Bi Pillay pia atashiriki mkutano wa tathimini ya mkataba wa Roma kuhusu mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC unaoendelea nchini humo. Baada ya kutoka Uganda juni nane mkuu huyo wa haki za binadamu ataelekea nchini Kenya.