Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la haki za binadamu limepiga kura ya kufnyika uchunguzi binafsi wa shambulio la Gaza

Baraza la haki za binadamu limepiga kura ya kufnyika uchunguzi binafsi wa shambulio la Gaza

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa leo limepitisha azimio mjini Geneva kulaani shambulio la Gaza na kutaka uchunguzi wa kina ufanyike.

Azimio hilo linataka iundwe tume huru maalumu kuchunguza shambulio lililofanywa na Israel dhidi ya boti ya flotilla iliyokuwa imebeba misaada kupeleka Gaza.

Baada ya siku mbili za majadiliano baraza hilo limepitisha azimio kwa njia ya kura. Wajumbe 32 wakiunga mkono azimio hilo, watatu wakipinga na wengine tisa hawakupiga kura kabisa.

(SAUTI :Eileen Chamberlan)