Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wapinzani Burundi wasema hawatoshiriki uchaguzi wa Rais Juni 28

Wapinzani Burundi wasema hawatoshiriki uchaguzi wa Rais Juni 28

Wapinzani kutoka vyama vitano nchini Burundi wleo wametangaza kuwa wanajitoa kwenye kinyang\'anyiro cha uchguzi wa Urais baadaye mwezi huu.

Wapinzani hao Agatho Rwasa kiongozi wa kundi la waasi wa zamani la FNL, Domitien Ndayizeye rais wa zamani wa nchi hiyo, Bi Paskalin Kamayano, Alexix Sinduhije na bwana Leonard Nyangoma.

Wote wanalalmikia kuwa uchaguzi wa wiki jana wa madiwani ulighubikwa na wizi wa kura na wanaona hakuna haja ya kushiriki uchaguzi wote. Mwandishi wetu wa Bujumbura Ramadhan Kibug anayo maelezo zaidi.