UNICEF inahitaji dola milioni 18 kusaidia watoto na wanawake DR Congo

UNICEF inahitaji dola milioni 18 kusaidia watoto na wanawake DR Congo

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema linahitaji haraka dola milioni 14 ili kukabiliana na mahitaji ya dharura ya watoto na wanawake Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

UNICEF inasema vita, ukatili dhidi ya raia, ubakaji, kuwaingiza watoto jeshini na maelfu ya watu kuuakimbia makazi yao kunazidi kuathiri sehemu kubwa ya Mashariki mwa nchi hiyo.

Shirika hilo linasema hata hivyo hali katika nchi nzima si ya kurudhisha. Kwa mujibu wa shirika hilo watu milioni 1.9 ni wakimbizi wa ndani na karibu asilimia 50 ni watoto.