Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wagombea watato wa Urais kutoka vyama vya upinzani wajiengua Burundi

Wagombea watato wa Urais kutoka vyama vya upinzani wajiengua Burundi

Nchini Burundi wagombea watano wa Uraia kutoka vyama vya upinzani wamejitoa kwenye kinyang\'anyoro cha uchaguzi wa urais utakaofanyika Juni 28 mwaka huu.

Hii ni baada ya vyama vya upinzani kulalamika kuwa uchaguzi wa madiwani wa wiki iliyopita ulighubikwa na wizi wa kura ambapo chama tawala cha CNDD/FDD kilijipatia ushindio mkubwa wa asilimia 64 ya kura zote.

Kujitoa kwa watu hao kutoa fursa kwa Rais wa sasa Pierre nkurunziza kusalia na mpinzani mmoja ambaye ni makamu wake wa Rais Yves Sainguvu kutoka chama cha UPRONA. Kutoka Bujumbura mwandishi wetu Ramadhani Kibuga anaarifu.

(SAUTI RAMADHAN KIBUGA)