Baraza la haki za binadamu linakutana kujadili shmbulio la Israel Gaza

1 Juni 2010

Baraza la haki za binadamu leo linafanya kikao maalumu mjini Geneva kuzungumzia operesheni za jeshi la Israel kushambulia boti ya flotilla iliyokuwa imebeba misaada kupeleka Gaza.

Katika mswada wa taarifa yake mkutano huo unatarajiwa kulaani vikali shambulio hilo lililokatili maisha ya watu na kujeruhi wengine wengi.

Taarifa hiyo pia inasema imesikitishwa na mauaji hayo ya raia wasio na hatia na pia inatoa rambirambi kwa familia za wafiwa na majeruhi waliokuwa kwenye boti hiyo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter