Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wajumbe kutoka nchi 180 wakutana Bonn kwa ajili ya mabadiliko ya hali ya hewa

Wajumbe kutoka nchi 180 wakutana Bonn kwa ajili ya mabadiliko ya hali ya hewa

Mzunguko mpya wa mkutano kuhusiana na mabadiliko ya hali ya hewa umeanza leo huku wawakilishi kutoka mataifa 180 wakikutana mjini Bonn Ujerumani.

Wawakilishi hao wanakutana ili kupeleka mbele kazi ya baada ya mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na mabadiliko ya hali ya hewa waa mwaka jana uliofanyika Copenhagen nchini Denmark. Lengo la mkutano wa Bonn ni kuangazia maswala ambayo hayakutatuliwa katika mkutano wa Copenhagen ili kutafutia njia ya utekelezaji wa juhudi za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

Mkuu wa mabadiliko ya hali ya hewa ya Umoja wa Mataifa Yvo de Boer amesema mkutano wa Copenhagen umehairisha matokeo kwa mwaka moja , lakini haujaahirisha athari za mabadiliko ya hali ya hewa