Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shirika la msalaba mwekundu linawasaidia walioathirika na kimbunga Agatha

Shirika la msalaba mwekundu linawasaidia walioathirika na kimbunga Agatha

Mvua kubwa zilizoambatana na kimbunga Agatha zimesababisha mafuriko Amerika ya kati na kufanya matawi ya mito kujaa kupita kiasi.

Athari nyingine ni pamoja na maporomoko ya udongo na miundombinu kuharibioka vibaya zikiwemo barabara. Hadi sasa taarifa kutoka nchi zilizoathirika zimethibitisha kuwa watu 82 wamefariki dunia Guatemala wengine 58 hawajulikani waliko na zaidi ya 81,700 wameathirika, 13 El Salvador na wengine zaidi ya elfu nane wamehamishwa, huku wawili wakiaga dunia Honduras kutokana na kimbunga hicho.

Shirika la msalaba mwekundu limekuwa likitoa msaada kwa waathirika na pia kufuatilia kwa karibu hali ya kimbunga hicho. Zaidi ya wafanyakazi wa kujitolewa 500 wanashiriki kutoa msaada nkutoka matawi 41 ya shirika hilo.