Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la haki za binadamu limeanza mkutano wake wa 14 mjini Geneva

Baraza la haki za binadamu limeanza mkutano wake wa 14 mjini Geneva

Mkutano wa kumi na nne wa baraza la haki za binadamu umefunguliwa leo mjini Geneva na kamishna mkuu wa haki za binadamu.

Katika ufunguzi kamshina wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu Navi Palley ameeleza baraza hilo kuhusu kazi zinazofanywa na  Ofisi yake.

Katika mkutano huo mukhtadha wa haki kuafikiwa kwa malengo ya milenia ya maendeleo, vita dhidi ya aina yeyote ya ubaguzi na kuwepo kwa haki ya maendeleo ni miongoni mwa mada zitakazojadiliwa.