Ban ameshiriki kandanda kuwakumbuka manusura wa vita nchini Uganda

Ban ameshiriki kandanda kuwakumbuka manusura wa vita nchini Uganda

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo amehitimisha ziatra yake nchini Uganda ambako alikwenda kufungua mkutano wa tathimini wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC.

Akishiriki mechi ya kandanda iliyoandaliwa mjini Kampala Uganda kwa kumbukumbu kwa waathiriwa wa vita, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ametoa heshima kwa manusura wa uhalifu wa kivita na vitendo vingine vya uhalifu. Ban amesena mlikabiliwa na vitenda vya kinyama lakini hamkukubali kuvunjika moyo na badala yake mlipambana kwa ujasiri na kuweza kurejesha heshima yenu.

(SAUTI YA BAN UGANDA)

Uganda ni mojawapo ya mataifa matano ambapo mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa Kivita ,ICC inaendesha uchunguzi kuhusiana na uhalifu wa kivita. Mahakama hiyo imetoa kibali cha kukamatwa kwa kiongozi wa LRA Joseph Kony, Okoth Odhiambo na Dominc Ogwen mwaka wa 2005 kwa shutuma ya uhalifu wa kivita na makosa dhidi ya ubinadamu, ikiwemo kuuwa, ubakaji na kuwasajili watoto kama wapiganaji.

Katika mechi hiyo timu ya Heshima iliyoongozwa na Rais Yoweri Museveni wa Uganda ilishinda dhidi ya timu ya Haki iliyoongozwa na katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.