Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamishna wa haki za binadamu ameshtushwa na shambulio la boti Gaza

Kamishna wa haki za binadamu ameshtushwa na shambulio la boti Gaza

Wakati huohuo kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameelezea kushitushwa kwake na shambulio hilo dhidi ya boti ya flotilla iliyokuwa imebeba misaada ya kibinadamu kupeleka Gaza.

Watu zaidi ya kumi ambao ni raia wamearifiwa kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya Israel kushambulia boti hiyo ilipokuwa njiani kuelekea Gaza. Amesema vizuizi vya Israel kwenye Ukanda wa Gaza vinakiuka haki za binadamu kila siku. Naye Imad Zumari kutoka Palestina amelaani shambulio hilo.

(SAUTI YA  IMAD ZUMAIRI)

Bwana Zumairi amesema kundi la nchi za Kiarabu na jumuiya ya nchi za Kiislamu watakutana ili kufikiria hatua za kuchukua.