Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu wa UM amelaani shambulio dhidi ya boti ya misaada Gaza

Katibu Mkuu wa UM amelaani shambulio dhidi ya boti ya misaada Gaza

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito wa kufanyika uchunguzi dhidi ya shambulio la boti iliyobeba misaada kupeleka Gaza na kukatili maisha ya watu.

Akizungumza mjini Kampala Uganda leo Ban amesema ameshtushwa na taarifa kuhusu mauaji hayo na kujeruhi wengine wengi. Watu zaidi ya 15 wameuawa katika shambulio hilo la mapema leo asubuhi .

Duru za habari zinasema majeshi ya Israel yameshambulia moja kati ya boti sita ambazo zilikuwa zikisafiri katika maji ya kimataifa. Ban amesisitiza ni muhimu kuwepo na uchunguzi wa kina kujua ni vipi mauaji hayo ymetokea. Ameongeza kuwa anaamini Israel ni lazima itoe maelezo haraka.