Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF inahitaji dola milioni 17 kwa ajili ya dharura nchini Zimbabwe

UNICEF inahitaji dola milioni 17 kwa ajili ya dharura nchini Zimbabwe

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema linahitaji dola milioni 17 ili kukabiliana na kuzuka kwa surua, kipindupindu na homa ya matumbo nchini Zimbabwe.

Shirika hilo linaonya kwamba watoto milioni tano wako katika hatari kutokana na kuzuka upya kwa siurua ambayo imeshawapata watoto elfu saba na wengine 400 wamearifiwa kufariki dunia tangu Septemba mwaka jana.

UNICEF na shirika la afya duniani WHO kwa pamoja wamezindua kampeni kubwa ya chanjo dhidi ya surua iliyoanza May 24 na itaendelea hadi Juni pili. Kuzuka kwa surua nchini humo kumetokea mwaka mmoja baada ya nchi hiyo kukumbwa na kipindupindu kibaya.