Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa NTP wamalizika kwa maafikiano ya mazungumzo ya Mashariki ya Kati

Mkutano wa NTP wamalizika kwa maafikiano ya mazungumzo ya Mashariki ya Kati

Mkutano wa mwezi mmoja wa kuzuia kuenea kwa silah za nyuklia umemalizika Ijumaa kwa makubaliano ya kuwa na mazungumzo ya kuanzisha eneo huru bila nyuklia Mashariki ya Kati.

Ni makubaliano ya kwanza katika muongo mmoja ya mkataba wa kuzuia silaha za nyuklia (NTP) ambao umeweka ajenda ya kimataifa ya kuzifanya nchi zisiweze kupata mabomu ya nyuklia tangu mwaka 1970.

Taarifa ya mwisho ya mkutano huo inataka ufanyike mkutano mwaka 2012 utakaohudhuriwa na mataifa yote ya Mashariki ya Kati ili kuongoza katika kuanzisha eneo huru la bila nyuklia.

Akizungumza kwa niamba ya nchi zisizofungamana na upande wowote ,mwakilishi wa Misri balozi Maged Abdelazizi amesema majadiliano yanajumuisha masuala mengi ambayo ni muhimu kwa mkataba huo