Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afisa wa Umoja wa Mataifa atoa tahadhari kuhusu hali ya jimbo la Darfur

Afisa wa Umoja wa Mataifa atoa tahadhari kuhusu hali ya jimbo la Darfur

Mratibu wa masual ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa anayezuru Darfur amesisitiza kuwa hali katika jimbo hilo la Sudan lililoghubikwa na vita ni mbaya.

Amesema mapigano ya karibuni baiana ya vikosi vya serikali na waasi yamekatili maisha ya watu wengi na kuwafanya maelfu kuzikimbia nyumba zao. Mashirika yasiyo ya kiserikali yamesitisha operesheni zake Mashariki mwa Jebel Marra kutokana na usalama mdogo.

Katika mkutano wake na kaimu gavana wa Darfur na maafisa wengine wa eneo la Nyaka mratibu huyo John Holmes amesisitiza haja ya serikali kuruhusu na kusaidia fursa ya mashirika ya misaada kuwafikia walengwa. Holmes katika ziara hiyo nchini Sudan pia ameelezea wasiwasi wake juu ya usalama wa wafanyakazi wa misaada kwenye jimbo la Darfur hasa masuala ya utekaji nyara wa wafanyakazi hao.