Skip to main content

Ban akaribisha msamaha kwa wapenzi wa jinsia moja nchini Malawi

Ban akaribisha msamaha kwa wapenzi wa jinsia moja nchini Malawi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye amekuwa nchini Malawi katika sehemu ya kwanza ya ziara yake barani Afrika baada ya kukutana na Rais Bingu wa Mutharika alihutubia.

Akuhutubia bunge Ban amesema wakati wa mazungumzo yake na Rais Bingu wa Mutharika ,rais huyo ametangaza kuwapa msamaha vijana wawili waliokua wakishiriki mapenzi ya jinsia moja.

(BAN CLIP MALAWI)

Steven Monjeza na Tiwonge Chimbalanga walitiwa hatiani mapema mwezi huu kwa kushiriki mapenzi ya jinsia moja na kuzusha mjadala mkubwa sehemu mbalimbali duniani ikiwepo kwenye Umoja wa Mataifa.