Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakati dunia ikiwaenzi walinda amani, maisha ya walinda amani yakoje?

Wakati dunia ikiwaenzi walinda amani, maisha ya walinda amani yakoje?

Wakati Umoja wa Mataifa na dunia ikiadhimisha siku ya walinda amani tunatathimini pia maisha ya walinda amani hao.

Wengi wanaishi katika mazingira ya mbali na nyumbani na familia zao, lakini kikubwa ni maisha wanayokabiliana nayo kila siku.

Kupata undani japo kwa kifupi maisha ya mlinda amani yakoje? Kapteni Paul kimiti raia wa Kenya anayehudumu na mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID mjini El-Fasher Darfur Sudan anatudokeza.