Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICRC inanunua mifugo ya Mali na Niger ili kuwasaidia wakulima wa nchi hizo

ICRC inanunua mifugo ya Mali na Niger ili kuwasaidia wakulima wa nchi hizo

Katika eneo la Agadez, Kaskazini mwa nchi ya Niger na katika eneo la Gao na Timbouktou, Kasakazini mwa Mali, Kamati ya Kimataifa la msalaba Mwekundu, ICRC linanunua karibu mifugo 38,000 kutoka kwa wafugaji 10,000 na familia za wakulima wanaoathiriwa na ukosefu wa usalama na kiangazi.

Kwa mujibu wa tathmini asilimia sabini ya mifugu inakabiliwa na hatari ya kuangamia kwa ajili ya kiangazi kinachokumba eneo la Sahel kwa wakati huu.

Mkuu wa ICRC katika eneo hili Jurg Eglin amesema ICRC inajaribu kuwasaidia watu wa kaskazini mwa Mali na Senegal wakati huu mgumu wa mpito