Skip to main content

MONUC sasa itaitwa MONUSCO bada ya vikosi hivyo kuongezewa mwezi mmoja

MONUC sasa itaitwa MONUSCO bada ya vikosi hivyo kuongezewa mwezi mmoja

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hivi leo limeongeza muda wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidekrasia ya Kongo, MONUC, kwa mwezi mmoja na kukubali kukifanya kikosi hicho kuwa cha kuimarisha hali nchini humo.

Kwa pamoja baraza hilo limesema kwa mujibu wa hali iliyofikiwa sasa Jamahuri ya Kidemokrasia Kongo, MONUC, kuanzia Juli 1 2010 kitakuwa kikosi cha uimarishaji wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo MONUSCO.

Muda wa MONUC utamalizika tarehe 30, mwezi wa June, ambapo baada ya hapo kikosi hicho kitaitwa MONUSCO,na muda wa MONUSCO utakwisha tarehe 30 mwezi wa June mwaka ujao.