Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM kufanya mashauriano kuhusu ukimwi na uhamiaji nchini Tanzania

IOM kufanya mashauriano kuhusu ukimwi na uhamiaji nchini Tanzania

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM wiki ijayo litafanya mashauriano nchini Tanzania kuhusu hatari ya kuambukizwa virusi vya ukimwi kwa watu wanaohamahama na jamii za mipakani.

Mashauriano hayo ya siku mbili yataanza Juni mosi na yataendeshwa kwa ushirikiano wa IOM, wizara ya mambo ya ndani ya Tanzania na tumeya kudhibiti ukimwi ya nchi hiyo TACAIDS. Yatawaleta pamoja wadau muhimu kutoamserikalini, jumuiya za kijamii, mashirika ya kimataifa nay a nchini humo, na wadau wa maendeleo ili kupeana mawazo ya njia bora ya kukabiliana na HIv kwa watu wanaohama na wanaishi mipakani.

Tanzania inapakana na nchi nane zingine za Afrika na pia ina mwambao wa pwani ya bahari ya Hindi unatumiwa kama mlango wa kuingi na kutoka kwa meli za mizigo za kitaifa na kimataifa, hususani bandari ya Dar es salaam.