Skip to main content

WFP imeonya juu ya ongezeko la tatizo la chakula kwenye ukanda wa Sahel

WFP imeonya juu ya ongezeko la tatizo la chakula kwenye ukanda wa Sahel

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP, limeonya dhidi ya ongezeko la idadi ya watu wanaohitaji chakula Mashariki mwa eneo la Sahel Afrika Magharibi.

Katika eneo hilo zaidi ya watu milioni 10 wanakabiliwa njaa kabla ya msimu wa mavuno mwezi Septemba kufuatia kutokana na mvua za masika kutonyesha inavyotakiwa.

Mkurugenzi wa WFP Magharibi mwa Afrika, Thomas Yanga amesema eneo la Sahel ni mojawapo ya eneo lililo na umaskini mkubwa ulimwenguni na hali ya njaa imesababisha watu wengi kutoka maeneo ya mashambani kuhamia mijini ili kuwatafuta chakula kwa ajili ya familia zao.

Ameongeza kuwa watu wamepoteza mavuno na mifugo na kwa hivyo kuchangia kuongezeka mara dufu kwa utapia mlo miongoni mwa akina mama na watoto.