Skip to main content

UNHCR yawasaidia maelfu ya Waghana walioko Togo baada ya kukimbia vita

UNHCR yawasaidia maelfu ya Waghana walioko Togo baada ya kukimbia vita

Mapigano makali kati ya wanavijiji katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Ghana yamewalazimu karibu watu 3,500 kukimbilia nchi jirani ya Togo kuanzia tarehe 18 mwezi uliopita.

Wakimbizi hao walikimbilia vijiji vinne katika wilaya ya Tanjouare katika eneo la Savane na wameliambia shirika la Umoja wa Mataifa la kuwashughulikia wakimbizi, UNHCR, kuwa nyumba na mali zao zimechomwa na kuharibiwa.

Kwa upande wake UNHCR limepongeza juhudi za serikali ya Togo za kuwapa wakimbizi hao chakula na mahitaji muhimu ya dharura japo tathmini ya UNHCR imeonyesha kuwa wakimbizi hao wanahitaji chakula, maji, nyumba na dawa.