Mapigano makali yameendelea kukatili maisha ya watu Moghadishu Somalia

Mapigano makali yameendelea kukatili maisha ya watu Moghadishu Somalia

Zaidi ya watu 7,000 wamelazimika kuzikimbia nyumba zao mjini Moghadishu Somalia kwa mwezi huu wa Mai pekee kutokana na mapigano makali yanayoendelea baiana ya vikosi vya serikali ya mpito na makundi ya wapinzani yenye silaha.

Watu wengine 14,300 walikimbia Moghadishu katika wiki mbili zilizopita baada ya kuzuka upya mapigano. Licha ya vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa afrika AMISOM kuvisaidia vikosi vya serikali hali ya mambo bado si shwari.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi limeelezea hofu yake juu ya kuongezeka idadi ya watu wanaopoteza maisha na wanaosambaratishwa na mapigano hayo hasa katika wiki mbili zilizopita.