Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nci za Afrika zimekutana kupambana na maambukizi ya HIv kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto

Nci za Afrika zimekutana kupambana na maambukizi ya HIv kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto

Wawakilishi kutoka mataifa 20 ya Afrika yaliyo na watu wengine wenye virusi vya HIV wanakutana Nairobi Kenya kujadili jinsi ya kukomesha maambukizi ya HIV kutoka kwa mama kwendda kwa mtoto ifikapo 2015.

Mkutano huo wa siku tatu unamalizika leo na umeandaliwa kwa ushirikiano na mfuko maalumu wa kupambana na ukimwi, kifua kikuu, na malaria na mashirika yaUmoja wa Mataifa yakiwemo la kupambana na ukimwi UNAIDS, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na shirika la afya duniani WHO.