Mchango wa walinda amani waenziwa Umoja wa Mataifa na duniani kote

Mchango wa walinda amani waenziwa Umoja wa Mataifa na duniani kote

Siku rasmi ya kimataifa ya walinda amani duniani ni Mai 29 lakini leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa na maeneo mbalimbali duniani waliko walinzi wa amani kumefanyika hafla maalumu ya unawaenzi na kuwakumbuka wale wote wanaojitolea katika nchi mbalimbali duniani kuhakikisha amani kwa wanaoihitaji inapatikana.

Kwenye makao makuu ya Umoja wa mataifa New York kumekuwa na hafla iliyoambatana na kuweka mashada ya maua kuwakumbuka waliopoteza maisha katika ulinzi wa amani kwenye nchi na matukio mbalimbali. Akiwa mjini Brazili Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameishukuru nchi hiyo na watu wake kwa kujitolea katika ulinzi wa amani na kuwaenzi walipoteza maisha wakati wa tetemeko la Haiti wakijitolea.

(SAUTI BAN KI-MOON)

Siku ya kimataifa ya walinzi wa amani ilianzishwa rasmi na mkutano mkuu wa UM mwaka 2002.Hata hivyo shughuli ya ulinzi wa amani inakabiliwa na changamoto mbalimbali kama anavyosema mmoja wa walinzi hao kutoka Darfur

(SAUTI EMMANUEL MOLELL)