Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi za afrika zakutana kutokomeza maambukizi ya HIV kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Nchi za afrika zakutana kutokomeza maambukizi ya HIV kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Wawakilishi wa serikali 20 za mataifa yaliyo watu wengi walioambukizwa Ukimwi barani Afrika wanakutana Nairobi kujadili jinsi ya kukomesha maambukizi ya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ifikapo 2015.

Mkutano huo wa siku tatu ulioanza jana na kumalizika kesho umeandaliwa kwa ushirikiano na mfuko maalumu wa kupambana na ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria na mashirika ya Umoja Mataifa yakiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwashughulikia watoto UNICEF, Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na shirika la Afya Duniani, WHO.

Washiriki watachambua jinsi ya kupanua na kutia uzito huduma kwa akina mama wajawazito pamoja na koungeza matibabu kwa akina mama na watoto waliathirika na virusi.