UNICEF kuwahamasisha vijana kwenye kombe la dunia dhidi ya dhulma

27 Mei 2010

Kabla ya mashindano ya Kombe la Dunia ya kandanda mwezi ujao Afrika Kusini, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linatumai kuwahamasisha vijana kujilinda dhidhi ya kudhulumiwa .

Kampeni hiyo ni kwa kushrikiana na kampuni ya simu ya MXit ambayo inatumiwa na vijana wengi wa chini ya miaka 18 nchini Afrika Kusini.

Kila mwaka maelfu ya watoto wanadhulumiwa kimapenzi kote duniani kila mwaka shirika la UNICEF likishirikiana na wadau wengine linapanga kuongeza juhudi zake katika kuwalinda watoto kufuatia hofu ya kudhalilishwa kwa watoto wakati wa mashindano hayo.

Kampeni hiyo ya kutoa kadi nyekudu itatoa taarifa kuhusu usafirishaji haramu wa watoto, picha za ngono pamoja na udhalilishaji wa aina nyingine pamoja na juhudi za kuwalinda watoto.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter