Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chad imeuhakikishia UM kuwa iko tayari kulinda raia wake baada ya vikosi kuondoka

Chad imeuhakikishia UM kuwa iko tayari kulinda raia wake baada ya vikosi kuondoka

Rais wa Chad Idris Debby amerejea ahadi yake kuwa serikali ya nchi hiyo itachukua jukumu la kuwalinda raia wake pamoja na wafanyi kazi wa mashirika ya kutoa misaada wakati ambapo shughuli za Umoja wa Mataifa zitakapo kamilika mwishoni wa mwaka huu.

katika mkutano wake na mratibu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mipango ya dharura John Holmes mjini Ndjamena siku moja baada ya Baraza al Usalama la Umoja wa Mataifa kupiga kura kuhitimisha shughuli ya kikosi chake cha kulinda nchini humo na Chad MINURCAT, kufuatia ombi la mataifa hayo, Debby amesistiza haja ya jumuiya ya kimataifa kulisaida taifa hilo kuchukua jukumu.

Katika ziara yake ya siku nne katika eneo la mashariki mwa Chad ambapo mamia ya maelfu ya watu wamekimbia makazi yao kufuatia mapigano ya wenyewe kwa wenye, katika nchi jirani ya Sudan jimbo la Darfur pamoja na mapigano yanayoendele magharibi mwa Sudan, amesema amejionea binafsi athari ya upungufu wa chakula na utapia

mlo.