Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yaelezea wasiwasi wake kuhusu kesi ya Omar Khadr Guantanamo

UNICEF yaelezea wasiwasi wake kuhusu kesi ya Omar Khadr Guantanamo

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwashughulikia watoto limeelezea wasi wasi wake kuhusiana na kuhukumiwa katika gereza la Gunatanamo Bay kwa mshtakiwa Omar Khadr.

Khadr alikamatwa Afghanistan mwaka wa 2002 kwa makosa inayokisiwa aliyatekeleza akiwa na umr wa miaka 15, likisema kuwa hii itaweka kiegezo hatari kwa watoto ambao wanasajiliwa kushiriki vita . Khadr ni askari mtoto wa mwisho anayeshikiliwa Guantanamo Bay, na kesi yake imemulikwa na maafisa wa Umoja wa Mataifa akiwemo Mjume Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto na mapigano Radhika Coomaraswamy.

Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF Anthony Lake amesema kwenye taarifa jana kuwasajili na kuwatumia watoto kwa vita ni kosa la kivita na walewanaohusika ni lazima washatakiwa.