Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umezindua kampeni kusaidia miji baada ya kukumbwa na majanga

UM umezindua kampeni kusaidia miji baada ya kukumbwa na majanga

Umoja wa Mataifa umezindua kampeni ya miaka miwili kuisaidia miji kuwa imara baada ya kukumbwa na majanga.

Lengo la kampeni hiyo ni kuwachagiza viongozi wa mabaraza ya miji ili wawekeze katika kupunguza athari za majanga. Kauli mbiu ya kampeni hiyo ni Mji wangu unajiandaa, je wako? Na inaongozwa na kitengo cha mpango wa kimataifa wa kupunguza majanga ya serikali ya Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa kitengo hicho athari za majanga ni kubwa katika miji kwa sababu ya mipango mibovu ya miji, msongamano katika maeneo ya mabanda na ukosefu wa miundombinu hususan wakati wa dhoruba. Mkuu wa kitenngo cha majana na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika kupunguza majanga ni Margaret Wahlstrom.