Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zingine mbili zimeridhiria mkataba wa CTB na kufanya idadi kuwa 153

Nchi zingine mbili zimeridhiria mkataba wa CTB na kufanya idadi kuwa 153

Jamhuri ya Afrika ya Kati na Trinidad na Tobago wameidhinisha mkataba unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ambao unapiga marufuku majaribio ya aina yeyote ya Nyuklia, na kwa hivyo kufanya idadi ya mataifa ambayo yameridhia mkataba huo kuwa 153.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema mkataba huo comprehensive Nuclear Test Ban Treaty, CTBT, ambao ilitiwa saini mwaka 1996 umetajwa kama kiungo cha msingi cha kuifanya dunia isiyokuwa na zana za nyuklia.

Wakati huo huo Ban amesema katika mkutano uliofanyika mwezi wa Septemba mwaka jana kuwa kuanzishwa kwa kanuni ya kimtaifa dhidi ya majaribio ya zana za nyuklia ,mkataba wa CTBT umetoa mchango mkubwa kwa jumuiya ya kimataifa katika juhudi za kuzuia usambazaji wa zana hizo.