Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

wanachama wa UM na makampuni waafikiana kufikisha huduma ya broadband mashuleni

wanachama wa UM na makampuni waafikiana kufikisha huduma ya broadband mashuleni

Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, makampuni makubwa ya kibinafsi ikiwemo kampuni ya kutengeneza kompyuta ya Microsoft wameahidi kupanua mtandao wa intanet wa broad band katika mashule ulimwenguni.

Nao Muungano wa teknolojia, ITU na Umoja wa Mataifa wakiwachagiza wengine kujiunga na juhudi hizo. Kampeni ya muungano huo wenye kauli mbiu unganisha shule, unganisha jamii, iliyozinduliwa mwaka jana ina lengo la kuunganisha mashule na huduma ya intanet ili shule ziweze kuhudumia jamii kama vituo vya teknolojia na mawasiliano, ICT.

Katibu mkuu wa ITU, Hamadoun Toure amesema lengo lao ni nikupanua huduma ya intanet ya broadband, na la muhimu wanahitaji kuzindua matumizi bunifu ya intanet kwa sekta ya afya, masomo,na biashara ili kusaidia katika kufikia malengo ya milenia yaani MDG's.