Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umedhidhishwa na hatua ya Marekani ya mswada wa kukabiliana na LRA

UM umedhidhishwa na hatua ya Marekani ya mswada wa kukabiliana na LRA

Akielezea maafa aliyojionea mwenyewe wakati wa ziara yake barani Afrika mratibu wa misaada ya Umoja wa Mataifa amepongeza kupitishwa kwa mswada wa Marekani wa kuwalinda raia dhidi ya waasi La Lord\'s Resistance Amry, LRA.

Kama mratibu wa misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa nimefurahia hatua ya Rais Barrack Obama ya kupitisha mswada huo, amesema John Holmes. Wakati wa ziara yake katika Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, mwezi uliopita , alizuru eneo la Niangara mahali ambapo LRA waliwauwa watu wengi na zaidi ya 280,000 kukimbia makazi yao mwezi Desemba.

Tangu mwezi Desemba 2007 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pekee karibu watu 1,800 wameuwawa, 2,300 wametekwa nyara na waasi wa LRA. 800 kati ya hao wakiwa watoto na wako katika hali ya dhiki sana.