Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa unasema amani inahitajika kunusuru wakimbizi Azerbaijan

Umoja wa Mataifa unasema amani inahitajika kunusuru wakimbizi Azerbaijan

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu na wakimbizi wa ndani Walter Kaelin amesema japo afueni inaongezeka kwa wakimbizi wa ndani Azerbaijan baada ya muda mrefu ni muhimu kuwa na muafaka wa amani ili kurejesha haki za binadamu za wakimbizi hao.

Kaelin ameysema hayo akiwa ziarani nchini humo na kuongeza kuwa amefurahu kurejea tena Azerbaijan ili kujionea mabadiliko yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitatu pamoja na changamoto zilizojitokeza.

Amesema amejionea mambo mengi yakuridhisha ktika ziara hiyo na serikali ya Azerbaijan imemuahidi kuwa suala la muafaka wa amani wanalichukulia kwa uzito na watalipa kipaumbele.