Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchumi wa dunia unaanza kuchipuka japo haumalizi tatizo la ajira

Uchumi wa dunia unaanza kuchipuka japo haumalizi tatizo la ajira

Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo inasema uchumi wa dunia umeanza kuchipuka tena kutoka katika mdororo japo ni polepole na haujafikia kiwango cha kupunguza matatizo ya ajira au kuzipa pengo la kuporomoka kwa uchumi.

Ripoti hiyo inasema mapato ya dunia yanatarajiwa kukuwa kwa asilimia 3.0 mwaka huu na alimilia 3.1 kwa mwaka ujao wa 2011. Hii itakuwa ni hatua kubwa kutoka asimilia 2.0 ya mwaka 2009. Hata hivyo ripoti hiyo iliyopewa jina la hali ya uchumi wa dunia na matarajio, iliyozinduliwa leo inasema bado kiwango cha kukua kwa uchumi huo ni polepole.

Imeongeza kuwa mafungu ya fedha za kunusuru vitu kama mabeni na kupanua sera za uchumi yamezisaidia nchi nyingi uchumi wake kukua kuanzia mwishoni mwa mwaka jana na mapema mwaka huu. Hata hivyo ripoti hiyo inasema bado juhudi zinahitajika ili kupandisha kiwango cha uchumi na kuzuia hali hiyo baadaye. Rob Vos ni kutoka DESA