Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afisa wa OCHA akamilisha ziara Chad na ameondoka kuelekea Sudan

Afisa wa OCHA akamilisha ziara Chad na ameondoka kuelekea Sudan

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya kibinadamu OCHA bwana John Holmes, amehitimisha ziara yake nchini Chad na ametoa ameagiza kupelekwa kwa haraka msaada kwa watu waliokumbwa na ukame nchini Chad.

Ombi lake limekuja baada ya kuzuru eneo la magharibi mwa Chad ambalo limeathirika vibaya na upungufu wa chakula na lishe bora. Kwa mujibu wa takwimu za tathimini ya chakula zilizotolewa hivi karibuni na shirika la mpango wa chakula WFP watu takribani milioni 1.4 wameathirika katika jimbo hilo la magharibi mwa Sahel.

Tathimini hiyo pia imeonyesha kuwa watu wapatao milioni 2 wako katika hatihati ya kukosa chakula nchini Chad. Akiwa ziarani nchini humo pia Hamekutana na Rais Idris Deby kuzungumzia masuala ya kibinadamu yanayowakabili watu wa Chad.

Holmes leo ataondoka kuelekea Sudan kwa ziara ya siku nne ambako angalia hali Sudan Kusini na kutathimini masuala ya kibinadamu kwenye jimbo la Darfur.