Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa walaani mauaji ya mbunge mpya nchini Iraq

Umoja wa Mataifa walaani mauaji ya mbunge mpya nchini Iraq

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Ad Melkert amelaani vikali kuuwawa jana usiku kwa Bashar Al Ouqeidi mmoja wa mbunge wapya wa Iraq mjini Mosoul.

Katika taarifa iliyotolewa leo Melkert ametumia familia ya Al -Ouqeidi rambi rambi zake huku akihimiza mamlaka nchini Iraq kuwasaka waliotenda kitendo hicho na kuwachululia hatua za kisheria.

Wakati huo huo Malkert amesema kitendo hicho cha kinyama hakitawavunja moyo raia wa Iraq katika azma yao ya kuwa na bunge na serikali mpya .