Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwanajeshi wa kulinda amani wa MONUC auawa Goma DR Congo

Mwanajeshi wa kulinda amani wa MONUC auawa Goma DR Congo

Mwanjeshi wa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, MONUC ambaye ni raia wa India ameuwawa baada ya gari lao la doria kuvamiwa na watu wasiojulikana kusini mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa MONUC baada ya kuona wanajeshi wa serikali wamevamiwa Kaskazini mwa Kivu , katika kile kinachosemwa ni mapigano ya mara kwa mara kati ya wanajeshi wa serikali na makundi ya waasi, kikosi hicho cha MONUC kilielekea kulisaidia jeshi la nchi hiyo na ndipo mwenzao aliposhambuliwa.

Mwanajeshi huyo alijeruhiwa katika majibizano ya risasi kasha akapelekwa hospitalini Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu na akafariki dunia baadae. Huyu ni mwanajeshi wa 31 wa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha Kulinda amani Congo MONUC kuuawa katika kipindi cha miaka 11 mpango huo wa MONUC kuwepo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.