Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban kuzuru Afrika akipigia upatu utekelezaji wa malengo ya milenia

Ban kuzuru Afrika akipigia upatu utekelezaji wa malengo ya milenia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea mipango yake ya kuzuru bara la Afrika mwaka huu.

Ban ameselezea changamoto zinazolikabili bara hilo wakati likijitahidi kutokomeza umasikini kwa kile kinachojulikana kama kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia (MDG'S) ifikapo mwaka 2015.

Ban amesema ziara yake Afrika itaanzia Malawi ambako atahutubia bunge la nchi hiyo, atakutan na Rais Bingu wa Mutharika ambaye ndio mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika, pia atazuru kijiji cha millennium ambako Umoja wa Mataifa unashirikiana na serikali, mashirika ya misaada na jumuiya za kijamii kuisaidia jamii kuondokana na umasikini uliokithiri.

Akitoka Malawi Ban ataelekea kampala nchini Uganda kufungua mkutano wa kwanza wa tathimini ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC iliyoundwa kama mahakama ya kudumu kuwahukumu watu wnaoshutumiwa kwa makosa ya uhalifu wa vita.