Ripoti ya maendeleo ya teknolojia 2010 imetolewa leo nchini India

25 Mei 2010

Reporti ya maendeleo ya teknolojia ya mwaka wa 2010 imezinduliwa hivi leo katika warsha ya maendeleo ya teknolojia inayofanyika mjini Hydarabad.

Repoti hiyo inatoa tathmini ya juhudi ya kuifanya dunia iwe jumuiya ya habari kufikia mwaka wa 2015, ahadi ambayo imetolewa na serikali kote duniani katika mkutano uliofanyika mjini Geneva 2003 na Tunisia mwaka 2005.

Repoti hiyo inaelezea ukuaji mkubwa wa sekta ya simu ya mkononi jambo ambali limepelekea kuunganishwa kwa maeneo mengi. Katibu mkuu wa muungano wa teknolojia duniani , ITU, Hamadoun Toure amesema takriban asilimia tisini ya watu ulimwenguni sasa wamuunganishwa kupitia simu za mkononi na kwa hivyo hata watu ambao wanaishi mashinani wana njia ya kuwasiliana na kujiunga na watu wa maeneo mengine.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter