Ukosefu wa fedha unatishia shughuli za misaada ya dharura Chad:FAO

25 Mei 2010

Ukosefu wa fedha unatishia shughuli za kutoa misaada ya dharura ya shirika la chakula na kilimo FAO nchini Chad.

Hayo yamesemwa leo wakati watu milioni mbili nchini humo wanakabiliwa na upungufu wa chakula kutokana na ukame na mimea kuliwa na wadudu, hali ambayo imesababisha kupungua kwa uzalishaji wa chakula.

Kwa mujibu wa mtaalamu wa operesheni za dharura wa FAO Fatouma Seid kufikia sasa FAO imeweza kuchangisha dola milioni mbili kati ya dola milioni 11.8 zilizoombwa mwezi Novemba mwaka jana kwa minajili ya dharura kwa ajili ya kilimo kama juhudi za pamoja za mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini humo.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter