Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikwazo dhidi ya Gaza ni athari kwa kilimo na wananchi wasio na hatia

Vikwazo dhidi ya Gaza ni athari kwa kilimo na wananchi wasio na hatia

Mashirika ya kutoa misaada yamechagiza serikali ya Israel kuondoa vizuizi vyovote vya uagizaji wa bidha zitakazochangia ukuuaji wa sekta ya kilimo na uvuvi kuingia na kutoka eneo la Ukanda wa Gaza.

Taarifa ya pamoja kutoka kwa mratibu wa misaada ya Umoja wa Mataifa ikiwakilisha mashirikia ya kutoa misaada na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali 80 , imesema tangu kuwekwa kwa vizuizi katika ukanda wa Gaza na serikali ya Israel mwaka wa 2007, uchumi wa Gaza umeanguka.

Mratibu wa misaada ya Umoja wa Mataifa katika eneo linalokaliwa la Palestina Philippe Lazzarini amesema kilimo na uzalishaji wa  vyakula vya kiasili katika ukanda wa Gaza untaegema mambo matatu Kufunguliwa kwa mpaka ilikuwapa fursa mashirikia ya misaada kuingia sawa na soko la kimataifa kwa bidhaa ya kilimo, kuwa na nafasi ya kutumia ardhi mihimu ya kilimo na uvuvi, na kulinda mchanga.

u