Mchakato wa uchaguzi mkuu umeanza leo Burundi kwa kura za udiwani

Mchakato wa uchaguzi mkuu umeanza leo Burundi kwa kura za udiwani

Raia wa Burundi leo wanapiga kura kuchagua madiwani katika awamu ya kwanza ya mchakato wa uchaguzi mkuu

Baada ya uchaguzi huu ili kukamilisha mchakato mzima uatafanyika pia uchaguzi wa bunge na wa Rais. watu zaidi ya milioni tatu wametarajiwa kushiriki uchaguzi wa leo ambao pia umeghubikwa na baadhi ya kasoro ikiwemo kuchelewa kwa vifaa vya kupigia kura vilivyosababisha uchaguzi huu uliokuwa ufanyike mwishoni mwa juma kuahirishwa hadi leo.

Mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo Charles Petrie amesema  Umoja wa Mataifa nchini humo umekuwa msitari wa mbele kusaidia ikiwa ni pamoja na kusambaza vifaa vya kupigia kurwa katika maeneo mbalimbali kwa kutumia elkopta. Amesema idadi kubwa ya watu wamejitokeza kwenye uchaguzi wa leo na kuonyesha ukomavu wa kisiasa kwa nchi hiyo iliyopitia machungu mengi.

Mwandishi wetu Ramadhan Kibuga amekuwepo mkoani Ngozi anakotoka Rais wa sasa Pierre Nkurunziza kushuhudia uchaguzi huo na kututumia taarifa hii.