Wataalamu wa uchafuzi wa mazingira wakutana Panama kutafita suluhu

Wataalamu wa uchafuzi wa mazingira wakutana Panama kutafita suluhu

Wataalamu 50 wa udhibiti wa uchafuzi wa mazingira kutoka nchi za Caribbean wameanza mkutano wa siku tano hii leo.

Mkutano wao unajadili jinsi ya kuzichagiza serikali kupunguza uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na taka zinazotupwa baharini. Mkutano huo unafanyika Panama City . Na nchini ya Panama inatafuta jukumu la kikanda la nchi kuridhia matakwa ya mkataba wa Cartagena ambao unatoa taratibu na viwango vya kikanda vya kupunguza athari za uchafuzi wa mazingira katika pani na mazingira ya majini na kwa afya ya binadamu.

Nchi 27 zinashiriki mkutano huo unaofanyika kwa mwaliko wa mpango wa mazingira wa Caribbean ulio chini ya UNEP ambao ni mpango wa mazingira wa Umoja wa Mataifa na shirika la kimataifa la masuala ya bahari IMO.