Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shambulio dhidi ya kasri la Rais laonyesha haja ya kutatua mzozo Somalia

Shambulio dhidi ya kasri la Rais laonyesha haja ya kutatua mzozo Somalia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon leo amesema shambulio la jana dhidi ya kasri la Rais nchini Somalia linadhihirisha haja ya haraka kutatua changamoto iliyopo nchini humo.

Akirejea mkutano wa Istanbul Uturuki uliokuwa ukijadili Somalia amesema ulikuwa ni muhimu hasa kwa wakati huu kwa Somalia. Amesisitiza kuwa Umoja wa Mataifa utakuwa msitari wa mbele kutoa msaada kwa Somalia ambayo imesambaratishwa vibaya na vita kwenye pembe ya Afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York leo Ban amesema mkutano wa Istanbul umetoa masuala matatu muhimu kwanza Umoja wa Mataifa hutatazama tuu na kuona Somalia ikiangamia peke yake. Pili amesema serikali ya mpito (TFG) ni lazime itimize wajibu wake na kutatua suala gumu la usalama na utawala. Na mwisho ameongeza kuwa kama hatutotatua chanzo basi itakuwa vigumu kukabiliana na uharamia pani ya Somalia.