Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban anaamini hatua zitakazochukuliwa na baraza la usalama dhidi yakuzama meli ya Korea

Ban anaamini hatua zitakazochukuliwa na baraza la usalama dhidi yakuzama meli ya Korea

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameunga mkono wito wa Rais wa Korea Kusini kuliaka baraza la usalama kufikiria kuchukua hatua dhidi ya Korea Kaskazini kwa kuzamisha meli yake.

Meli hiyo iliarifiwa kugongwa na torpedo mwishoni mwa mwezi Machi na mabaharia 46 wa Jamhuri ya Korea waliuawa katika ajali hiyo. Ban akizungumza na waandishi wa habari hii leo amesema kutokana na wito wa Rais Lee wa korea Kusini kwa baraza la usalama kuchukua hatua dhidi ya tukio hilo , majadiliano ya faragha yanatarajiwa baiana ya wanachama wa baraza la usalama.

Ameongeza kuwa tukio hilo linakumbusha uharaka wa kuwa na amani na utulivu katika ghuba ya Korea. Pia amesema licha ya tashiwshi hii iliyojitokeza Umoja wa Mataifa utaendelea na shughuli zake za msaada kwa wale wanaouhitaji katika Jamhuri ya watu wa Korea.