Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID imethibitisha kuwepo mapigano baiana ya serikali ya Sudan na JEM

UNAMID imethibitisha kuwepo mapigano baiana ya serikali ya Sudan na JEM

Mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kwenye jimbo la Darfur Sudan UNAMID umethibitisha kuwepo kwa mapigano baina ya vikosi vya serikali ya Sudan na waasi.

Kwa mujibu wa UNAMID hali ni ya wasiwasi na vikosi vya serikali vilekuwa katika mapambano na kundi la Justice and Equality Movement (JEM) karibu na eneo la Um sauna kilometa 65 kusini mwa Darfur.

Mapigano hayo yaliyoanza Mai 19 yamekatili mjaisha ya watu wengi na wapiganaji kutoka pande zote. Taarifa zinasema pande hizo hasimu zimeafiki kuruhusu mashirika ya misaada katika uwanja wa mapambano ili kuchukua maiti. Ibrahim Gambari ni mkuu wa UNAMID